Mwanarepa chipukizi toka hapa mombasani Johnzy aliyewachapia vibao kama 'I want more, Panda na Own cash, hivi sasa amewachilia kibao kipya kijiulikanacho kama 'Naitinga'.
Ngoma hii ni ya nguvu na imewavutia wengi hasa vijana kwa mtindo wa trap beat. Johnzy anatarajia kuwachia video hiyo wakati wowote kwani bado iko maandalizini. "Natarajia kufanya kitu tofauti na wasanii wengi wanavyofanya." Ndivyo anavyoeleza mwanarepa huyu.
Ngoma zake zina patikana sound cloud na reverbnation. Msanii Johnzy ameweza kushirikiana na wasanii chipukizi kama vile Mykwillar, Lil Jos na Topgunz. Nasi tuko tayari kuwaharifu mapya yatakayojiri.
No comments:
Post a Comment