Mwanarepa chipukizi toka hapa mombasani Johnzy aliyewachapia vibao kama 'I want more, Panda na Own cash, hivi sasa amewachilia kibao kipya kijiulikanacho kama 'Naitinga'.
Ngoma hii ni ya nguvu na imewavutia wengi hasa vijana kwa mtindo wa trap beat. Johnzy anatarajia kuwachia video hiyo wakati wowote kwani bado iko maandalizini. "Natarajia kufanya kitu tofauti na wasanii wengi wanavyofanya." Ndivyo anavyoeleza mwanarepa huyu.
Ngoma zake zina patikana sound cloud na reverbnation. Msanii Johnzy ameweza kushirikiana na wasanii chipukizi kama vile Mykwillar, Lil Jos na Topgunz. Nasi tuko tayari kuwaharifu mapya yatakayojiri.
Thursday, 6 October 2016
Rapper Johnzy awachia ngoma mpya.
Wednesday, 5 October 2016
Chikuzee awachia ngoma mpya na Kevz Ally
Baada ya mda mchache bila kutoa ngoma mpya ,mkali wao zee la mavuvuzela(chikuzee) ameamua kufanya collabo na msanii chipukizi anaye kuja kwa kasi kevz Ally toka ghetto bitz chini ya usimamizi wa meneja mkubwa sasa..
Mashabiki wameweza kuulizia ngoma hiyo inatoka lini lakini bado kibao hicho kipo jikoni thunder sound recordz .
Wengi wana imani collabo hii itakuwa yanguvu nasi kama talanta pwani tuko chonjo kuwa fahamisha yatakayo jiri toka kwao hao wasaniii.
Pwani tv yawika
Wakazi wa pwani wajivunia stesheni ya pwani tv kwa kuwapa habari na burudani murwa. Wasanii chipukizi wa pwani wanafurahia stesheni hii vile vile kwa kuweza kupewa fursa ya kuonekana kwenye runinga.
Pata habari na burudani kem kem kwenye stesheni hii kupitia masafa ya kidijitali. Hongera wana pwani.
Tuesday, 4 October 2016
Dj Lyta afanya mambo
Dj Lyta azidi kunawiri katika safu ya sanaa nchini na hata barani Afrika. Anatarajiwa kuja hapa pwani baada ya show yake ya kericho.
Monday, 3 October 2016
Kutana na produza Amadoo
Prodzer wanguvu aliye anza mziki ghetto bit hivi sasa ameza kupata fursa ya kwenda nairobi nakufanya kazi na mkali wao link produzer.
Saturday, 1 October 2016
Meet the music Samorai aka VJ VAN
Meet the finest Dj Van aka the music Samorai who does his things uniquely. He likes mixxing dancehall music. Catch him on whispers media while he does his things.